GET /api/v0.1/hansard/entries/1462305/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1462305,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462305/?format=api",
    "text_counter": 153,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nakumbuka tulipokuwa wachanga, baba na mama walikuwa wafanyikazi wa Kitengo cha Afya. Walikuwa wakifanya kazi kwa Serikali. Ingawaje tulikuwa wachanga, tulikuwa tunaona dhiki na shida katika hali ya maisha. Ukweli wa mambo tukiwa tunaunga mkono Statement ya Mheshimiwa ni kwamba, mara nyingi magavana wa Kenya wakishughulikia mipango ya afya, hawaangalii shida na changamoto za wafanyikazi katika kitengo cha afya. Mara nyingi, wanashughulikia mijengo. Lakini ikifika mahali pa kushughulikia wale wafanyikazi wa serikali za kaunti kwa upande wa afya, wanawachilia sehemu hiyo. Kwa hivyo, ninaunga mkono hiyo Statement kwa sababu saa hii, wafanyikazi wa afya wa Meru wamegoma kwa sababu ya shida na kutojaliwa na mamlaka ya Gavana wa kaunti hiyo. Kwa hivyo, nimesimama hapa kuunga mkono Statement hiyo. Tuangalie na tuwafanyie haki wafanyikazi wa serikali. Katika familia yetu tulipokuwa wachanga, kama baba na mama hawangetoka kwa Serikali na kwenda kufanya private practice, najua tungekuwa tumeishi maisha mengine tofauti kama vile waliobaki kufanya na Serikali. Bi. Spika wa Muda, maombi yangu ni kwamba upande wa afya pia upewe pesa za kutosha. Na tusiseme haiwezekani, inawezekana. Wengine wetu ambao tumefanya katika kitengo cha haki miaka iliyopita, tulikuwa tunajua kwamba, mawakili ambao walikuwa wanafanya upande wa Serikali, hawakuwa wanalipwa vizuri. Mara nyingi, tulipokuwa tunaanza kazi, sote tulikuwa tunakimbilia upande wa kufanya kazi kibinafsi ama privatepractice kwa sababu huko ndiko tulikuwa tunajua kuna hela. Lakini, miaka hii iliyokuja baadaye, tumeona Serikali inalipa mawakili wao vizuri. Prosecutor na Director of Public Prosecutions (DPP) wako sawa. Hakuna tofauti kubwa kati ya wale ambo wanafanya kazi kwa serikali na wale ambao wanafanya kazi za kibinafsi ama private practice. Ukweli wa mambo ni kwamba, kama Serikali imeweza kufanya vile kwa upande wa mawakili na sheria, hakuna sababu nzuri ya kutosha ya kutofanya hivyo kwa wafanyikazi wa kitengo cha afya. Kwa hivyo hakuna sababu ya sisi kusema kwamba magavana wasifanye hivyo. Bi Spika wa Muda, ninasema hivi kwa sababu ya shida ambayo iko Tana River Kaunti. Maombi yangu ni kwamba, wakati Kamati ya Afya ya Seneti itakaa kuangalia suala hili, waangalie pia sehemu ya Tana River Kaunti. Wafanyikazi wetu wana mishahara duni. Wafanyikazi katika kaunti zingine wanapata mishahara mikubwa kushinda wale wa Tana River Kaunti. Hii inaleta mgogoro kwa sababu utakuta watu wengine wanatoroka ile kaunti ili wakafanye kazi katika kaunti zingine ilihali, wote wamefanya training sawa. Kwa hivyo, suala hili liangaliwe na Kamati ya Afya. Waulize kwa nini Council of Governors (CoG) hawawezi ku- standardise . Ikiwa wewe unafanya kazi ya nurse kwa kaunti hii, uwe pia unalipwa mshahara sawa na wale wanafanya kwa kaunti zingine. Kwa nini tusiwe na structure ambayo itasimamia Kenya mzima, kaunti 47, ili wafanyikazi wawe wanapata mishahara ya sawa? Jambo lingine pia ni promotion ya hawa wafanyikazi wa Serikali. Kuna kaunti ambazo watu wanacheleshwa promotion na zingine, wanafanyiwa haraka na haieleweki ni kwa sababu gani. Kwa hivyo, naomba wakati ambao Statement hii inaangaliwa, CoG pia, waitwe ili wajieleze kwa nini hawawezi kuwa na structure ambayo itakuwa inafanya mambo ya promotion katika gatuzi 47."
}