GET /api/v0.1/hansard/entries/1462306/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1462306,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462306/?format=api",
    "text_counter": 154,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kule kwetu Tana River, kuna wale ambao waliajiriwa kazi katika kitengo cha afya kwa contract . Katika kaunti zingine, contract hizo zimeanzishwa upya ama zimekuwa extended na wamekuwa absorbed . Lakini katika kaunti yetu, wale ambao wamefanya kazi na contract hawajakuwa absorbed . Swali ni; kwa nini kaunti zingine wanafanya hivyo ilhali zingine wafanyikazi hawapewi zile contract zinazotakikana. Sisi tunaomba kuwe na standardisation ama usawazishaji wa mambo ya haki za wafanyi kazi wa afya katika Kenya mzima na gatuzi zote za Kenya. Bi. Spika wa Muda, katika Statement hiyo na kutokana na mambo yanayofanyika katika kaunti yangu, kwa sababu ya kukosa kuwapatia wale wafanyikazi extendedcontract, kuna kitu kinaitwa understaffing ama ukosaji wa wafanyi kazi wa kutosha katika health department . Watu wengi wakienda hospitali, wanakuta pengine yule ambaye ni mkubwa wa hospitali ndiye clinical officer na tena yeye ndiye anasimamia records . Kuna shida katika hizi dispensaries kwa sababu wale ambo walikuwa wapewe hizi extended four-yearcontracts, hawakupewa, ilhali kaunti zingine wamekuwa absorbed . Kwa hivyo, ninaomba wakati Kamati ya Health itaangalia, pia waangalie sehemu zingine kama Tana River Kaunti. Bi. Spika wa Muda; poor working conditions . Mtu anaenda kufanya kazi, anataka kipimo cha damu kifanyike na akienda kule, hakuna reagents ama dawa zinazotakikana ili hiyo damu ikipimwa, ilete majibu ambayo daktari atafanyia kazi. Mtu anatumwa lab ilhali hakuna reagents . Kwa pharmacy, hakuna zile dawa ambazo zingefaa zimsaidie yule mgonjwa baada ya kuonwa na daktari. Tunataka Kamati ya Afya ya Senate waangalie pia sehemu zingine, sio Meru Kaunti pekee. Waangalie kuna shida gani katika kaunti zingine kama vile Tana River County ili wakati wanatoa uamuzi, watoe uamuzi wa kutosha. Kweli, wafanyikazi wengine wa Serikali kule Tana River Kaunti wamepata nyumba lakini, ni nyumba za zamani. Zilijengwa wakati wa ukoloni na ukweli ni kwamba, nyingi zinaporomoka. Hakuna namna ama budgets ambazo zinawekwa kusaidia kutengeneza nyumba hizi ili wafanyikazi wa pale wawe wanafanya kazi vizuri. Mfanyikazi wa hospitali yuko pale kazini lakini hata vyoo haviko safi wala katika hali ya kutumika. Mtu akiwa anafanya pale hospitali, inabidi arudi nyumbani akiwa na mwito wa haja."
}