GET /api/v0.1/hansard/entries/1462486/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1462486,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462486/?format=api",
"text_counter": 55,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw. Spika. Kwa niaba ya Bunge la Seneti na Maseneta watatu kutoka Gatuzi za Pwani, tukiongozwa na Sen. Faki, ningependa kuwakaribisha kaka zangu, MCAs waliochaguliwa kutoka Jimbo la Mombasa; Bw. Anza Fresh kutoka Old Town na Bw. Patrick Mbelle kutoka Bamburi Ward. Ningependa hii iwe ni ufunguzi wa kuwaleta wale MCAs wengine ili waje washuhudie yale ambayo tunayatendea kazi hapa katika Bunge hili. Mjihisi mko nyumbani kwa sababu majukumu yetu yako sawa; kulinda raslimali ya mkenya. Nawaomba mjihisi mko nyumbani na wakati wowote, milango ya Bunge la Seneti iko wazi ili tuweze kubadilishana fikira kwa kuiendeleza mbele taifa letu la Kenya. Asante."
}