GET /api/v0.1/hansard/entries/1462564/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1462564,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462564/?format=api",
    "text_counter": 133,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Sen. Osotsi amesema vizuri kwamba unapata wengine wanaanguka na kufariki kwa sababu ya mshtuko wa roho, kwa kujitolea. Katiba yetu ya Kenya inasema kiwango fulani cha kazi kipewe watu fulani. Unapata wengine ni vilema na vijana ambao hawana zile pesa na wamekopa, halafu mali yao ile kidogo waliokuwa nayo inauzwa. Kama vile Seneta wa Bungoma alivyosema, ukitembelea sehemu hiyo, utapata ule Uga wa Masinde Muliro uliotengenezwa na mwanakandarasi anayejulikana kama Ruwao. Ametumia zaidi ya Kshs150 milioni na gatuzi lenyewe halijaweza kumlipa kitu chochote. Hili ni jambo ambalo si la kawaida na limekuwa mazoea. Hapa Seneti tunaongea na hakuna lolote linalofanyika. Tunapaswa tusiliongelelee tu, bali tuchukulie watu kadhaa hatua ndio iwe funzo. Katika Seneti tunagawa pesa kuenda kwa gatuzi zetu na hakuna jambo linalotendeka kwa sababu ya madeni. Sio Kaunti ya Bungoma pekee yake, ukitembea Kaunti ya Laikipia, mambo ni yale yale. Bw. Spika, kuhusu Taarifa iliyoletwa na Seneta wa Nairobi, watu wamekuwa chonjo na ngangari. Niliona wananchi wakimtimua Gavana wa Nairobi kwa sababu alienda kuwaambia pole na hakufika kwa wakati uliofaa. Gari la wazima moto ndilo lilipaswa kutangulia kuzima ule moto. Niliwasikia Wakenya wakisema ya kwamba gari halikuweza kufika."
}