GET /api/v0.1/hansard/entries/1462578/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1462578,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462578/?format=api",
"text_counter": 147,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, nikinukuu usemi wa mwenzagu, tungependa pia kujua miradi iliyofanywa na wale wanaodai. Tungependa kujua walijenga zahanati gani katika kaunti zetu au walipeana huduma za aina gani. Tungependa pia kujua magavana wanatumia mbinu gani kulipa baadhi ya wanakandarasi na kubakisha wengine. Naomba kupeana mfano wa mama kutoka Kaunti ya Bungoma. Mama huyo alikuwa anapeleka bidhaa katika Soko la Kamukuywa. Alilia ili alipwe deni lake. Hatimaye alifariki. Jambo la kusikitisha ni kuwa hadi leo, familia yake haijalipwa."
}