GET /api/v0.1/hansard/entries/1462579/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1462579,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462579/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ningependa kujua kwanini tunaweka Wakenya katika hali ngumu. Wanachukua mikopo ili kufanya biashara na serikali za kaunti. Licha ya kuwa Serikali inatuma pesa kwenda katika kaunti zetu, bado watu wanahangaishwa bila kulipwa madeni yao. Kama Seneta wa kike mchanga, najua kuwa vijana wa kiume na kike wanajaribu. Wangependa sana kufanya biashara na Serikali lakini wanaingiwa na uoga wa kuchukua mikopo katika taasisi tofauti tofauti ili kujihusisha katika biashara na Serikali. Ningependa sisi kama viongozi turekebishe tabia hiyo ili tulisukume gurudumu la Serikali yetu mbele."
}