GET /api/v0.1/hansard/entries/1462625/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1462625,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462625/?format=api",
    "text_counter": 194,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, asante kwa nafasi hii. Kwanza, nawapa pole walioathirika na janga la moto katika soko la Toi. Hili ni jambo ambalo lazima tuangazie kama Seneti. Ni vipi magatuzi yetu yamejiandaa katika kukabiliana na janga la moto? Jambo la kusononesha sana ni kwamba baadhi za kaunti za Kenya hazina magari za kuzima moto na vifaa mahususi vinavyoweza kutumika kuzima moto. Janga linapotokea, wao ni kushika simu kuuliza moto ulianza wapi, unafanana namna gani, watu wamejaa au la, barabara inapitika au haipitiki, ilhali mali ya watu inachomeka na maisha kuangamia. Jumba la Seneti liangazie kujiandaa kwa kaunti zetu katika kukabiliana na majanga ili mali ya wanabishiara wa Kenya isije iharibike. Jambo la pili ni Hoja iliyoulizwa na Mhe. Beth Syengo kuhusiana na vyuo vikuu. Tunapoangazia miundo mbinu na jinsi vyuo hivi vinafadhiliwa, ni jambo la kusononesha sana katika kaunti zetu. Juzi tumekuwa na Gavana wa Kaunti ya Bungoma na wanaotia sahihi matumizi ya pesa, baadhi ya akaunti zao za benki hawajulikani. Ni ishara kwamba tusipoangaza macho jinsi pesa zinavyotumika, baadhi ya vyuo hivi vitatumika kama ng’ombe za kiuchumi ambazo zitakamuliwa kwa niaba ya Wakenya. Mwisho kabisa ni kuwarai Maseneta wenzangu kwamba wakati umefika Serikali inapokaza kamba kuhakikisha utepetevu na kutolewa katika idara ya mawaziri kadhaa tuliyonao hata katika sekta ya wizara na kaunti zetu. Tuhakikishe kwamba ugatuzi na fedha inatumika ipasavyo."
}