GET /api/v0.1/hansard/entries/1462692/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1462692,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462692/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, Hazina ya Kitaifa ni National Treasury. Sasa sijui nimfunze Kiswahili ama nichangie mada. Ukiangalia katika Kamusi ya Kiswahili sanifu, mfuko ni fund kwa lugha ya Kiingereza. Kwa hivyo, Sen. Cherarkey, sijakosea chochote. Utajifunza mengi kutoka kwangu. Hesabu inayotumika kutenga fedha ni ya Mwaka 2020/2021 ambayo ndio ya karibu sana ilipitishwa na Bunge la Taifa. Mbali na kuwa pesa hizo ni chache sana kulingana na jinsi mapato ya Serikali yamekuwa, sasa tuko katika Mwaka 2024/2025 ambapo mapato yake ni tofauti na yale yaliyopatikana Mwaka 2020/2021. Jambo la pili ni kwamba pesa hizo zinatakiwa ziwe nusu ya mapato. Kwa hivyo, hawawezi kukaa katika Bunge la Taifa na kusema kuwa Serikali imetenga Kshs10,867,400,000 na kupunguza Kshs790 milioni ili ibaki Kshs10,077,400,000. Kiwango hicho kimewekwa na Katiba. Hivyo basi, Wabunge hawana mamlaka ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}