GET /api/v0.1/hansard/entries/1462693/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1462693,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462693/?format=api",
    "text_counter": 262,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "kupunguza Kshs790 milioni ili ibaki Kshs10,077,400,000. Hicho ni kinyume na Katiba. Sisi kama Seneti hatuwezi kukubali hilo. Jambo la tatu ni kwamba tangu hazina ya usawa ianzishwe, ni juzi tu, mwaka 2021, nilipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Endelevu, yaani Committee on Delegated Legislation. Tuliweza kupitisha kanuni zinazotumika sasa kuendesha hazina hii. Kwa miaka kumi, hazina hii haikuwa na kanuni za kuendesha fedha hizo. Walipeleka kanuni zilizokataliwa na mahakama. Hivyo basi, kwa miaka kumi, miradi ilifanya bila malipo kwa sababu ya ukosefu wa sheria endelevu za kuhakikisha Hazina hii inafanya kazi. Ni masikitiko kwamba mpaka sasa, Hazina hii haijasaidia sehemu zilizotelekezwa kwa muda mrefu. Kwanza zilikuwa kaunti 14 na sasa ni 34. Nina hakika tukiangalia mfumo wa mgao wa mara ya tatu, labda Kenya nzima itakuwa na sehemu zilizotengwa. Kwa mfano, Kaunti ya Kiambu ina utajiri mkubwa na matajiri wengi. Hata hivyo, kuna sehemu zilizotelekezwa katika kaunti hiyo. Ugatuzi uliletwa ili kuleta usawa katika kaunti zetu. Hata hivyo, sehemu nyingi zimetelekezwa kwa sababu pengine hawakukubaliana na Gavana aliye mamlakani ama Mwakilishi wa Wadi wa eneo fulani hana uhusiano mzuri na gavana. Kwa hivyo, ni muhimu hazina hii itumike kwa mujibu wa Katiba ili kuleta usawa. Kwa sababu imekiuka Katiba, lazima tukatae mapendekezo hayo---"
}