GET /api/v0.1/hansard/entries/1462829/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1462829,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462829/?format=api",
"text_counter": 398,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, kwa ufupi sana, naunga mkono Mswada huu wa sheria mpya inayosimamia walimu katika shule za chekechea. Hivi majuzi, watu kadhaa waliajiriwa kazi katika Kaunti ya Tana River. Watu walifurahia kwa sababu watu wengi hawana kazi lakini mishahara ya hao walimu waliopata hizo kazi na kufurahia iko chini sana. Sheria hii tunayoileta leo itasaidia walimu wale kupata mishahara inayofaa zaidi kwa maisha yao. Mwalimu anashinda na watoto wadogo kutoka asubuhi mpaka jioni lakini pesa anayopeleka nyumbani mwisho wa mwezi ni kidogo. Nashukuru sana kwamba leo nimepata fursa hii, kwa niaba ya watu wa Kaunti ya Tana River, kupitisha sheria hii mpya itakayosaidia walimu wa Early Childhood Development (ECD) wapate mshahara zaidi. Bw. Spika, kwa hayo mengi, naunga mkono Mswada huu wa sheria hii mpya. Asante."
}