GET /api/v0.1/hansard/entries/1462937/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1462937,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462937/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Maseneta, ni lazima tuweze kuamua ikiwa tunataka kwenda ile njia ya kamati au Seneti nzima ambapo Maseneta wote wanachangia katika Hoja hii iliyo mbele yetu. Najua Bunge la Seneti linajulikana kwamba lipo na Maseneta majabali, maseneta ambao wanaweza kuketi wakasikiza kesi na kukata kisawasawa. Sintofahamu ni kwamba pengine kukatokea cheche za maneno kutoka nje na kunakuwa na lawama tofauti tofauti kulinganishana na Maseneta wetu. Hizo huwa ni cheche tu. Tunaelewa kwamba cheche zingine ni kama maji moto, haiwezi kuchoma nyumba. Kwa hivyo, hawawezi kutuambia maneno yanayowezafanya tukose mwelekeo na pengine tusikate kesi kulingana na zile stakabadhi zilizowekwa hapa mbele; stakabadhi tutakazojadiliana nazo kuona kwamba hatua iliyochukuliwa ni ile kila Mkenya ataona kwamba haki imefanywa na Wabunge wa Seneti. Kwa hivyo, njia itakayochukuliwa ni ile ambayo sisi sote tutafuatilia. Sote tuko hapa, tutajadiliana na kuona ni njia ipi tunafaa kuelekea. Naunga mkono hii Hoja kwamba ni sawa kabisa. Asante."
}