GET /api/v0.1/hansard/entries/146294/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 146294,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/146294/?format=api",
    "text_counter": 246,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, sikuwa nimemaliza. Nilipewa dakika mbili tu. Kwa hivyo, naomba nichukue dakika zangu kumi. Kama hapo awali nilipokuwa nimesema, tunamshukuru Naibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha kwa mchango wake ambao ametoa wakati wa kutoa ratiba ya fedha za Serikali. Nilizungumza kwa kirefu na nikajazia kuwa mna mambo kadha wa kadha ambayo tungependa yafafanuliwe na yaelezwe vile yatakvyokuwa yakitekelezwa. Kama tulivyosomewa Makadirio ya Fedha za Serikali, ilibainika wazi kuwa fedha nyingi zinapelekwa kwa Wizara na haifafanuliwa waziwazi jinsi Wizara hizo zitatumia fedha hizo. Tukiangalia shughuli ambazo ziko za Wizara, tuna wasiwasi huenda Wizara zikawa ni chanzo cha kushikilia fedha hizo ili zisiende katika shughuli ambazo zinatakiwa. Tunaomba wakati huu, Wizara zisiwe ni pingamizi za kuzuia fedha zisiingie katika shughuli za utekelezaji wa kazi. Shughuli zingine ni za barabara. Tumeona kuwa mwaka huu Makadirio ya Fedha yameonyesha wazi nia ya Serikali ya kuhakikisha kuwa muundo msingi nchini umetekelezwa Lakini wasiwasi wetu ni kuwa huenda fedha hizi pia zikaenda sehemu fulani na zingine zikaachwa. Tungeweka mkazo kuwa wakati huu, kwa sababu tumejua katika visa vya 2007 moja ya matatizo tuliokuwa nayo ni kuwa wananchi walikuwa"
}