GET /api/v0.1/hansard/entries/146296/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 146296,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/146296/?format=api",
    "text_counter": 248,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wanaona kuna sehemu zimestawi kuliko zingine na ilikuwa inaletwa na ugawaji mbaya wa fedha. Tunaomba wakati huu kama barabara zitatengenezwa, angalau tuangalie nchi yote bila kuwa na ubaguzi ama kupendelea sehemu fulani. Na nikiwa nachangia jambo hili, naangalia barabara kama ya Taveta-Voi. Tukiangalia Kaskazini ya Tanzania, mali yote ya Tanzania ikifika Moshi hadi Holili inaenda Dar-es-Salaam. Kutoka Holili hadi Dar-es-Salaam ni kilomita 650. Kutoka Holili hadi Mombasa ni kilomita 250. Nchi yetu inapoteza biashara yote ya Tanzania kwa sababu ya njia fupi tu ambayo ni kilomita 110 kutoka Voi hadi Taveta. Tunaomba wakati huu, barabara hiyo ishughulikiwe. Tunashukuru pia kuwa hospitali zimepatiwa fedha kama Kshs20 milioni katika kila sehemu ya uwakilishaji. Tunaomba pia wakati huu, hela hizo zitumiwe sawasawa kustawisha hospitali. Ukiangalia hospitali ya wilaya yangu, utaona kwamba imedidimia; hali yake ni mbovu. Hamna wauguzi au wataalam ama madaktari. Kwa maana wakati huu Wizara zimeagizwa kuajiri madaktari na wafanyikazi wengine, ni matarajio yangu kuwa hospitali hizi zitapatiwa madaktari wa kutosha. Mradhi wa Kazi kwa Vijana unaendelea lakini tunaomba pia ifafanuliwe wazi Kazi kwa Vijana inafanya namna gani, nani anaajiri hao vijana, ni nani anahikikisha kuwa fedha hizi zimelipwa vijana, ni kazi gani ambazo zinafanywa, nani amekaa chini akaweka ratiba ya kazi ambazo zitafanywa kwa vijana? Hatukatai ni Wizara lakini je, Wabunge wanahusishwa ama zimekuwa pia ni mbinu za kutumia fedha ama hela za Serikali kuhakikisha kuwa wale maofisa wa Serikali ndio wanatumia hela hizi. Bw. Naibu Spika, tukiangalia mambo ya wanyama, tungependa mikakati iwekwe sawasawa na Serikali kuona kuwa wenzetu, hasa wale ambao wanashughulika na mifugo, wakati kama huu wa kiangazi, ni nini kinafanywa kuhakikisha kuwa maji yapo ya kutosha, wanyama wapate maji, kusije kukawa na shughuli kama tunayoiona hivi sasa; ng’ombe hawana maji na wanazurura kila mahali. Hivi sasa, kuna mzozo baina ya wanyama wa pori na mifugo, hasa ile ya wenzetu kutoka Mkoa wa Kaskazini. Mifugo yote imeingia katika Wilaya ya Taita! Tutafanya nini? Ng’ombe wanafukuzwa kutoka mbuga za wanyama. Wanafukuzwa waiende wapi? wameingia mashambani mwetu. Tutawafanya nini? Na sisi tutawafukuza! Tutawafukuza waende wapi – mbugani ama wataenda wapi? Jambo hilo linaleta utata kati ya wananchi na ndugu zetu ambao wanafuga ng’ombe kutoka sehemu za Kaskazini. Tungependa angalau wakati huu, Serikali iwe inafikiria mambo kama haya yatashughulikiwa namna gani na yashughulikiwe kikamilifu. Sio kiholela."
}