GET /api/v0.1/hansard/entries/1462985/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1462985,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1462985/?format=api",
"text_counter": 111,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw. Spika. Kenya, kuna Kaunti ya Meru ambayo iko na wapiga kura takribani elfu mia nane. Leo sio siku ya kwanza kuongea kuhusu mambo ya Kaunti ya Meru. Leo ni mara ya tatu. Nashangaa sana nikisikia wenzangu wakisema tuchague Kamati ya watu kumi na moja. Kaunti zote arobaini na saba nchini Kenya zitafuatilia tutakavyoamua kesi hii ya Kaunti ya Meru. Kwa miaka miwili, watu wa Meru wamehangaika na kuumia. Hii sio mara ya kwanza Gavana Kawira Mwangaza kuletwa hapa. Hii ni mara ya tatu. Wakati aliletwa hapa mara ya pili, tulimpatia onyo. Katika Bibilia, kitabu cha Isaya, sura ya kwanza, msitari wa kumi na nane, unasema, “Haya njoni, tusemezane, asema Bwana”. Tulimwambia aende aongee na makanisa, Members of Parliament (MP)na Members of County Assembly (MCAs ) na wasemezane waone jinsi watasaidia Kaunti ya Meru. Sasa ni mara ya tatu analetwa kwetu. Kama Seneta wa Kaunti ya Embu, naunga mkono tusikilize Hoja hii tukiwa Maseneta sitini na saba kwa sababu tuko na ujuzi wa kuamua kama amefanya makosa kwa mara ya tatu au la. Sioni kwa nini hawa MCAs wanaweza kuwa wanamuekelea gavana Kawira Mwangaza mashtaka usiku na mchana. Ni vizuri tuangalie kama atakuwa amefanya makosa, atimuliwe na Maseneta sitini na saba, na kama hajafanya makosa, arudishwe. Asante."
}