GET /api/v0.1/hansard/entries/1463032/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1463032,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1463032/?format=api",
"text_counter": 158,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Bw. Spika, ningependa kuchukua fursa hii kuchangia mjadala huu unaohusu watu wa Meru. Napinga Hoja hii kwa sababu si vizuri kuwachia Maseneta 11 kuamua hatima ya watu wa Meru ikizingatiwa kuwa hii ni mara ya tatu kwa Gavana huyo kuletwa katika Seneti. Jambo hili linafaa kuangaziwa na Seneti nzima ili kutoa uamuzi. Maseneta 67 wataangazia jambo hili kwa kina na kwa njia itakayosaidia wakaazi wa Kaunti ya Meru. Kuna mambo ambayo Gavana wa Meru ameshtumiwa kufanya. Tukiwa na vikao hapa, mambo hayo yatakuwa yanaangaziwa si na Kenya pekee bali ulimwengu mzima. Watu watakuwa wakifuatilia ili kuona uamuzi wa Seneti. Bw. Spika, napendekeza kuwa jambo hili liangaziwe na Seneti nzima ili kila mtu ajue hatima ya Gavana wa Meru, Mhe. Kawira Mwangaza, na watu wa Meru wapate haki."
}