GET /api/v0.1/hansard/entries/1463071/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1463071,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1463071/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono ili kikao hiki kiwe cha wale Masenetea 11 waliochaguliwa. Hii ni kwa sababu wale ambao hawakuweza kuchaguliwa na wananchi wataweza kupata fursa ya kutoa kauli zao. Tutakapo ingia kukiskiza kikao hiki kwa pamoja, sisi kama wawakilishi tulioteuliwa na vyama vya kisiasa hatupati fursa ya kupiga kura na sauti yetu huwa haisikiki. Kwa hakika, watu wa Meru wamekuwa katika mtihani mkubwa. Hii kamati itakuwa mzuri kwa sababu maswala yao yatasikizwa kwa ufasaha zaidi. Nasema hivi kwa sababu niliweza kukaa katika kikao kama hiki cha Gatuzi la Siaya. Kwa kweli, tulipokuwa katika Kamati ya Maseneta 11, nilipata fursa ya kuuliza maswali kwa undani. Mara ya mwisho tulipokuwa tumeketi hapa kwa pamoja kama kikao cha Seneti na Maseneta 67, nilipata fursa moja tena ya madakika kidogo kuuliza swali katika mjadala uliokuwa unaendelea. Kwa hivyo, kama Seneta wa Mombasa, napendekeza na kumuunga mkono Sen. Sifuna ili tuweze kuwaachia majukumu haya wale Maseneta 11 waliochaguliwa kusikiliza kesi ya watu wa Meru na haki ipatikane. Asante."
}