GET /api/v0.1/hansard/entries/1463755/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1463755,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1463755/?format=api",
"text_counter": 90,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": " Ninazungumza kuhusu mtu anayejaribu kujitoa uhai ama anayetaka kujitia kitanzi. Kabla mtu hajaamua kujiua ama kujitia kitanzi, kuna sababu ambazo huenda zimemfikisha afanye maamuzi hayo. Huenda ikawa ni ugonjwa au shida ya kiakili. Tunafaa kutofautisha hayo mambo mawili. Katika Bibilia, Mwenyezi Mungu anasema hatufai kujiua ama kuwaua wenzetu. Mtu hastahili kujitia kitanzi, kujitoa uhai, ama kuua mtu mwingine. Kuna mambo mawili hapa: kujitoa uhai au kujitia kitanzi ama kumuua mwingine. Mtu aliye na ugonjwa wa kiakili anafaa kupelekwa hospitalini ilia apate tiba. Kwa hivyo, tukisema yule mtu anajaribu kujitoa uhai, kujitia kitanzi ama kumtoa uhai mwingine, anafaa kupelekwa hospitalini. Lakini kuna wengine ambao kutokana na hasira au chuki, wanaweza kuwatoa uhai wenzao. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}