GET /api/v0.1/hansard/entries/1464257/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1464257,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1464257/?format=api",
    "text_counter": 138,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohamed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Ninachukua fursa hii kuwapongeza hawa wanawake wawili ambao wameteuliwa katika nyanja mbalimbali. Kenya ilikuwa imeenda sehemu mbaya. Pia, ninachukua fursa hii kumpongeza Rais wa Taifa hili, Mhe. William Samoei Ruto, kwa kuleta uwiano katika taifa. Hii imekuwa sababu ya sisi kupata wanawake wazuri na shupavu ambao wana uweledi wa kazi. Wao ni maono ya wanawake katika Kenya nzima. Pia, tukizingatia zile theluthi tatu ambazo tulikuwa tunatafuta kama akina mama, mimi nina hakika kuwa hawa akina mama, Ms Beatrice na Ms Dorcas, watafanya kazi zao kulingana na Katiba. Palipo na uongozi wa akina mama, hata maji huwa yanapanda mlima. Kwa hivyo, ninachukua fursa hii kuipongeza ile Kamati iliwateua na kuwapitisha. Ninakushukuru sana, Mhe. Spika. Nilifuatilia kwa kina Kamati hii. Ulipeleka mambo hayo kwa uweledi sana, na hukuangalia hivi ama vile. Uliangalia ule msimamo ambao wale walikuwa nao na mkawapitisha. Kwa hivyo, ninawaombea dada zangu. Ninawambia wafanye kazi ili wajenge taifa. Wasilemee upande mmoja. Wafuate sheria ili tuone uongozi wa wanawake unaoleta mabadiliko katika taifa. Ninawaombea Mungu aweze kuwapa nguvu na aghari ya kuweza kufanya kazi bila kuangalia huku na kule. Asante sana, Mhe. Spika."
}