GET /api/v0.1/hansard/entries/1467729/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1467729,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1467729/?format=api",
    "text_counter": 2601,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, katika kanda za video ambazo tumeonyeshwa hapa, tulimwona Gavana Kawira akisema kuwa kuna pesa ambazo zimechangwa. Hii ilinikanganya kidogo kwa sababu alipokuwa akinena kwa lugha ya Kimeru alisema kuwa pesa zilizokusanywa ni shilingi milioni 87. Lakini alipozungumza kwa lugha ya Kiswahili alisema pesa zilizokusanywa ni shilingi millioni 60 na akasema zinaweza tumika kumjengea nyumba ya ghorofa yule mjane na vilevile anunuliwe gari. Bw. Spika wa Muda, katika kanda nyingine ya video, nilimsikia MCA akisema kuwa Gavana wa Meru County ni wazimu. Lakini, baadaye alipokuwa akiulizwa kuhusu swala lile alisema kuwa alinukuliwa vibaya. Mimi nashindwa kama ni yeye alimnukuu Gavana wa Meru na kusema kuwa amesema mambo mawili ambayo hayaambatani. Kwanza, pesa zilizokusanywa ni shilingi milioni 87 tena kwa Kiswahili, nikaskia akisema kwamba, yeye alinukuliwa vibaya. Inaonekana waziwazi ya kwamba amesema mambo mawili tofauti. Akiongea kwa lugha ya Kimeru, alisema tofauti na yale yaliyosema akiongea kwa lugha ya Kiswahili. Yeye mwenyewe anaweza kusema ya kwamba alinukuliwa vibaya katika ile tuhuma ambayo imeletwa katika Seneti hii. Nashukuru."
}