GET /api/v0.1/hansard/entries/1469723/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1469723,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1469723/?format=api",
    "text_counter": 1308,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Mnamo tarehe 16/10/2023, wakati tulikuwa tukiangalia Hoja iliyokuwa imewasilishwa hapa kuhusu kung’atuliwa kwa Gavana Kawira, Mhe. Mawira ambaye yuko mbele yetu alikula kiapo. Aliweka hati ya kiapo ambayo alikuwa amechukua kusema kwamba ana akili timamu na ana uweazo wakuaminika na akatia kidole, ile hati ya kiapo aliyoleta katika Seneti. Leo, chini ya kiapo, ameleta pia, hati ya kiapo kingine, ambayo imebadilisha mawazo na kusema ya kwamba, hii Seneti ilikaa chini kuangalia makaratasi, tukapoteza pesa za umma na wakati, kufuatilia stakabadhi ambazo zilikuwa hazina maana."
}