GET /api/v0.1/hansard/entries/1470405/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1470405,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1470405/?format=api",
"text_counter": 1990,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante Bw. Spika. Gavana Kawira, swali langu ni moja tu kuhusu yule mshauri wako kwa mambo ya sheria anayeitwa Linda Gakii Kiome. Ulimuajiri kazi kama mshauri wako wa mambo ya sheria tarehe ishirini na nane, mwezi wa tatu, mwaka wa elfu mbili ishirini na tatu. Mwaka mmoja kamili baadaye, tarehe ishirini na sita, mwezi wa tatu, mwaka wa elfu mbili ishirini na nne, ulimpatia barua ya kumuachisha kazi. Je, baina yako na yeye, kulikuwa na kukosana, tabu, ama kutoelewena fulani ndio sababu akasema kwamba sio yeye aliyeandika ile barua, bali ile barua iliyoandikwa, si wewe uliyetia sahihi. Nataka kujua hayo tu."
}