GET /api/v0.1/hansard/entries/1471453/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1471453,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1471453/?format=api",
"text_counter": 97,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika, asante sana kwa kunipa fursa hii. Mwanzo, nampongeza Bw. Douglas Kanja kwa kuteuliwa kuwa generali mkuu wa polisi. Ni vizuri ijulikane wazi, Kanja anapokuja, aje akijua kwamba kazi kuu ya Serikali yoyote ni kulinda mali na maisha ya wananchi. Bw. Spika, ukitembea sehemu nyingi za Bonde la Ufa, hasa Laikipia County, utapata wakati mwingi watu wanaishi kwa maisha ya kukimbizwa na kuibiwa na wezi wa mifugo. Ningependa kumuuliza Generali wa Polisi atakapoingia, azingatie na kukubalia tuongeze askari wetu wa ziada, kwa Kingereza wanaitwa National Police Reservists (NPR). Hii ni kwa sababu hawa ndio askari walio na uzoefu na ujuzi katika mahali ambapo wametoka. Vile vile, hao askari wanapaswa kuangaliwa na kushughulikiwa kwa sababu wakati mwingi wanapouawa huwa hawapati faida yeyote. Ningependa wao na familia zao wapewe National Hospital Insurance Fund (NHIF) iwe ikiwashughulikia wakati wanatapa matatizo, hasa ya magonjwa. Nikiangalia ripoti iliyoletwa mbele yetu, nimefurahi kuona ya kwamba, utajiri wote wa Inspekta Generali ni shilingi milioni 46. Tungependa baada ya mwaka mmoja tuangalie utajiri wake utakuwa umepanda kiasi kipi kwa sababu kila wakati tunaona mtu anaingia katika ofisi kuu za Serikali, utajiri wake unaendelea kuongezeka zaidi. Hio ni ahadi moja ya kupigana na ufisadi. Ufisadi ni lazima ungaliwe kwa kiasi cha haja. Sehemu zingine ambazo tungependa kumuambia anapoaingia ni, kwa mfano, Bonde la Ufa, wakora wengi wanabunduki kinyume cha sheria. Kwa hivyo, anapaswa aungane na maafisa wale wengine wa ujasusi na jeshi ili waweze kuwanyanganya wale watu walio na bunduki kinyume cha sheria. Hii ni kwa sababu hizi bunduki ndizo zinahangaisha watu wengi wanaoishi katika sehemu hizo. Bw. Spika, ukitembea Kaunti ya Laikipa mahali panaitwa Ol Moran, Wangwashi, Miteta na Ethituna utaona kuna shida ya usalama. Ninafahamu na kujua ya kwamba, ataweza kuifanya kazi yake kwa ujasiri na bila kuogopa chochote kwa sababu huyu afisa ni mtu ambaye amebombea katika kazi yake. Nikiangalia alianza kufanya kazi ya usalama kwa muda mrefu. Bw. Spika, nchi yetu tuna kumbwa na magaidi, na kwa sababu yeye aliongoza katika oparesheni ya fagia Boni, najua atasaida zaidi. Tumekuwa na shida ya pombe katika sehemu nyingi nchini Kenya. Watu wanakisia ya kwamba maafisa wengine wa polisi wanamiliki bars na wanaendeleza mambo ya kuuza pombe. Kwa hivyo, anapaswa kushughulikia hayo mambo ya mgongano wa kiraslimali. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}