GET /api/v0.1/hansard/entries/1471454/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1471454,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1471454/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Kwa mambo ya maandamano yaliyokuwa yakifanyika katika nchi ya Kenya, sisi tulitoa mwongozo hapa na tukapitisha vile ambavyo Serikali inapaswa kufanya. Kwa hivyo, hatuna haja ya kujisumbua kumuuliza huyu afisa. Anapaswa kufuata mambo ambayo tulielekeza katika Bunge hili. Tulisema ya kwamba, wale waliouawa wanafaa kufidiwa na Serikali. Vile vile, tulisema walioko kwa hospitali pia wanapaswa kufidiwa. Ningependa kusema nampongeza huyu afisa. Tukiangalia historia yake, ni mtu aliye na uzoefu, sina shaka. Namtakia kila la heri katika jukumu mpya alilopewa la kuongoza askari wetu. Tunajua ya kwamba, baada yamuda aliopewa, tutaona kazi atakayaokuwa ameifanya."
}