GET /api/v0.1/hansard/entries/1472390/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1472390,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1472390/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Spika. Nami ninatoa rambirambi zangu, za familia yangu na watu wa Lamu kwa jumla, kwa Mheshimiwa aliyefariki. Ningependa pia kuchukua nafasi hii kutoa rambirambi zangu kwa familia ya Naibu wa Gavana wa Lamu aliyefariki. Mungu aiweke roho yake pahali pema. Alikuwa mtu mzuri mwenye ukakamavu na maskini amewacha familia ndogo. Mwenyezi Mungu aisaidie familia yake na ajaze pengo alilowacha. Kwa Gavana wetu wa Lamu na wakaazi wa Lamu, mwenyezi Mungu atupe subira na badali. Mungu amwezeshe Gavana kufanya uamuzi wa busara. Ninatoa pole kwa watu wa Mpeketoni, familia na watu wote wa Lamu kwa niaba ya familia yangu na watu wa Lamu Mashariki. Tumepoteza mtu muhimu lakini Mungu anampenda zaidi."
}