GET /api/v0.1/hansard/entries/1472839/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1472839,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1472839/?format=api",
    "text_counter": 200,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta Kaunti, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangia mjadala huu ambao unamjadili mteule wa kuwa Inspekta Mkuu wa Polisi. Naanza kwa kuipongeza Kamati ambayo imeandika Ripoti hii na kutuletea hapa. Nimeona Ripoti ni nzuri sana. Wamemchunguza vyema na kutuletea Ripoti nzuri. Huyu Bwana Douglas Kanja Kirocho ni mzoefu kwa kazi yake. Alianza kazi hii kwenye daraja dogo; amepanda madaraka mpaka akafikia mahali amefika. Hivyo ndivyo tunataka kuona watu wakipanda vyeo kama hivyo na kuungwa mkono wakiwa wamefanya vyema. Tulimjua kwa ubora wake sana akiwa katika oparesheni ya janga la bomu pale Dusit D2. Kwa kweli alifanya kazi nzuri na vyema kabisa. Lingine ni kwamba hatujamsikia akitajwa katika mambo ya ufisadi. Tumejua shirika la polisi limekuwa likitajwatajwa na kuhusishwa sana na mambo mengi ya ufisadi. Kwa miaka yote hiyo amekuwa katika shirika hilo, hajahusishwa. Hilo pia ni jambo jema na la kupigiwa upato. Kwa hivyo, naungana na wenzangu kuunga Ripoti hii mkono na kumtakia kila la heri atakapopata fursa ya kuwa Inspekta Mkuu katika taifa letu la Kenya. Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa."
}