GET /api/v0.1/hansard/entries/1472842/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1472842,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1472842/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia North, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Sarah Korere",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "mwanakamati wa Kamati hii, tulimhoji Inspekta Mkuu wa awali. Ukweli ni kwamba, umahiri na ukakamavu aliyonao bwana huyu katika kuyatekeleza majukumu yake ni wa hali ya juu sana. Aliitikia wito wake, maanake kuwa askari pia ni wito, kwa umri mchanga. Alifanya kazi katika sehemu kama Lokichogio, Kapedo na kwingineko. Hamna anayeelewa vizuri zaidi hali ya usalama kaskazini mwa nchi yetu na pale ambapo hali ya usalama imetukera sana sisi wenyeji kama Bw. Kanja. Alipokuwa Naibu Inspekta Mkuu, ilikuwa rahisi mno kumfikia kuliko kumfikia kamanda wa polisi katika kaunti yako. Kwa hivyo, anastahili na anaweza kazi. Sio kwa sababu anatoka mahali fulani au kwa sababu ako na jina fulani, ni kwa sababu ni Mkenya ambaye anapenda nchi yake na ameihudumia kwa ukakamavu na unyenyekevu. Kwenye masuala ya elimu, kosi ambayo huyu bwana amehitimu ikilinganishwa na shahada anaweza kuwa pia na shahada ya uzamifu (PhD) kwa masomo yake kama polisi. Nchi hii inahitaji polisi watakaohudumia wananchi. Polisi ni huduma. Ninaamini huyu bwana atayatekeleza hayo. Kando na hayo, mara nyingi tunajipata sisi viongozi na wananchi tukiwalimbikizia polisi lawama chungu nzima kwa sababu ya kutotekeleza majukumu yao. Lakini tunakosa kufahamu kuwa mara nyingi hata kwenye Bunge, tunapotengenza Bajeti, pesa wanazotengewa polisi ni kidogo sana. Ndio maana kama mwanakamati wa Kamati hii, tunapokuwa na matarajio chungu nzima, lazima polisi wapewe zile fedha zitakazowawezesha kutekeleza majukumu yao. Mara nyingi usalama ukiharibika, kila mtu anahukumu polisi, haswa kwenye masuala ya haki za kibinadamu. Mimi huwa nauliza swali moja: Polisi siyo binadamu na hana haki? Unatuma polisi kutekeleza wajibu wake lakini hana nguo rasmi ya kumkinga dhidi ya kurushiwa mawe na hana vifaa vya kutosha anavyohitaji. Unataka afanye aje? Tunapoongelea haki za kibinadamu, lazima tuelewe kwamba polisi wana haki. Hao polisi siyo polisi tu bali ni binadamu. Hamna kiwanda cha kutengeneza polisi ila sisi tunaozaa watoto ndiyo viwanda. Ni watoto wetu na ndugu zetu. Kwa hivyo, lazima tuwachunge vizuri ili wawe na motisha ya kulinda haki na usalama wa Kenya vizuri. Usipompatia mtu haki yake, hamna yeyote atakayepeana asicho nacho. Ukimpa haki, atakupa haki. Ukimnyima haki yake, nawe usitarajie kupata haki kutoka kwake. Naunga mkono haya mapendekezo. Nawaeleza viongozi wa Kenya kuwa tuna shida nyingi ila kujua nani anatawala mlima siyo moja wapo. Viongozi wa nchi hii lazima waiunganishe. Iwapo yale tunaona, kwamba watu fulani wamekuwa viongozi wa sehemu fulani yataendelea, basi hatuna budi kubadilisha Katiba ili kila jimbo kati ya yale majimbo yaliyokuwa nane liwe na Naibu wa Rais, ndio tupate watu wa kuzungumzia Kenya nzima. Sio mtu anayezungumzia mlima kila siku kuanzia asubuhi hadi jioni. Kenya iko na mlima, Bonde la Ufa, Pwani na kadhalika."
}