GET /api/v0.1/hansard/entries/1473149/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1473149,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1473149/?format=api",
"text_counter": 240,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Kwanza, naunga mkono Hoja hii ya kugeuza Kalenda yetu ya Seneti. Kunazo sababu zinazofanya tugeuze Kalenda hii. Kwanza, ile tarehe iliyowekwa ya Seneti Mashinani imebadilika hadi mwezi wa Kumi na Moja. Vile vile, Maseneta watapata nafasi ya kujiandaa kusafiri kuenda Busia kwa ratiba ya Seneti Mashinani. Natoa ushauri kwamba ni lazima tuzingatie seriousness katika Bunge la Seneti. Kuna hizi tabia tunazozianza za kutoa hoja za nidhamu wakati Seneta mwezako anapoongea na pengine hujapenda anachoongea. Seneta anasimama ama kubofya kile kidude kilichoko mbele yake na kusema anataka kutoa hoja ya nidhamu. Hoja ya nidhamu ninavyoielewa kwa wakati nimekuwa hapa ndani na ndugu yangu, Sen. Cheruiyot na Sen. M. Kajwang’, ni kitu cha muhimu. Bw. Spika wa Muda, hoja ya nidhamu ni kitu muhimu sana na kuingilia mtu katikati akiwa anaongea, inapoteza mwelekeo ama zile fikra alizokua nazo. Tuweze kujizuia na tumwache yule anayeongea, aongee mpaka amalize halafu ndio utajua mwelekeo wake ulikua namna gani. Hoja ya nidhamu ni sawa lakini tuitumie kwa njia ya kisawasawa. Hayo ndio maoni yangu ninayosema. Cha mwisho ninachoona ni cha muhimu ni kwamba tunaenda Senate Mashinani na kutakua na watu wengi kule. Ukiangalia hapa ndani, utapata Maseneta walio hapa ni wadogo kuliko ile nambari inayotakikana. Nikikumbuka ile Seneti ya kwanza ya 2013, ilikua inajaa sana, mpaka ikifika Saa Kumi na Mbili na Nusu jioni, bado Maseneta wamejaa humu ndani. Ni ukweli kabisa na saa zingine ukweli ukisemwa, unakua uchungu. Bw. Spika wa Muda, tukiangalia ndani ya hii Seneti, tunaona tumepoteza mwelekeo. Ninaomba ndugu zangu, ni muhimu tukiwa hapa ndani tujifundishe ili waliokuja sasa hivi waweze kujua. Mtu kama Mhe. (Dr.) Boni Khalwale huketi hapa mpaka mwisho kila siku. Hiyo hatuwezi kataa. Ndugu yangu, Mhe, Sifuna, anaketi hapa mpaka mwisho na hatuwezi kataa hiyo. Ningependa kuuliza wale wengine, haswa Maseneta wapya ni lazima waweze kujua. Hata Sen. Gloria pia yuko pale na yeye huketi mpaka mwisho ikiwa kuna sababu. Lakini ana zile tabia zingine ambapo anaingia hapa ndani--- Sitaendelea na pande hiyo lakini asije na vile vitisho vyake vya kuvaa namna gani na kujipaka rangi sijui gani."
}