GET /api/v0.1/hansard/entries/1473230/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1473230,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1473230/?format=api",
"text_counter": 321,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono kubadilisha kwa tarehe ya kuwa na kikao katika Kaunti ya Busia. Hii inapatia Seneti fursa ya kutembea mashinani ili kuchangamkia mambo yanayowahusu watu katika ile kaunti. Haijapotea kwangu kwamba Seneti hii imetembea katika kaunti nyingi. Tumetembea Kaunti ya Kitui ambapo tuliona kwamba Gavana alikuwa ametengeneza kiwanda cha kutengeneza nguo wakati ule. Tulienda Uasin Gishu tukaona wakulima wamejawa na ghadhabu wakati ule wakisema kwamba wanataka bei yao ya mahindi iangaliwe. Nakumbuka Mhe. Murkomen aliambiwa “wacha Kiingereza. Una Kiingereza kizuri lakini leo ongea mahindi.” Tukienda mashinani tunaweza kupata haya mambo moja kwa moja kutoka kwa wananchi. Vile vile, tulitembelea hospitali ya Moi Referral Hospital na tukaona shida zinazowakumba. Hivi juzi tumekuwa katika Kaunti ya Turkana. Kama kamati, tuliweza kuona vile stima inavyotengenezwa pale na maswali mengi yaliibuka. Kwa hivyo, vikao katika gatuzi zetu vinapatia Seneti fursa ya kuungana na wananchi, kuulizwa maswali na wananchi moja kwa moja na kuona mambo yanavyotendeka pale mashinani. Shughuli yetu kubwa kama Seneti ni kuangalia mambo pale mashinani. Naunga mkono kubadilishwa kwa tarehe ijapokuwa nilikuwa nimejipanga vizuri kwa zile tarehe zilikuwa zimewekwa. Mzungu anasema kwamba ni mtu mpumbavu tu asiyebadilisha mawazo. Asante."
}