GET /api/v0.1/hansard/entries/1473425/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1473425,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1473425/?format=api",
"text_counter": 90,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Ningependa kukosoa Seneta wa Nairobi ambaye ni rafiki wangu. Waziri Mbadi sio wa Kenya Kwanza, hivi sasa Serikali ni ya muungano. Kwa hivyo, kupigia sisi kelele na kusema kuwa Waziri huyu ni wa Kenya Kwanza ni makosa makubwa. Pili, wakati tulipitisha swala la Mawaziri kuja Bungeni kujibu masawali, ulikuwa nje na hukutuunga mkono. La mwisho, Waziri Mbadi amefanya makosa, angekuja ili tumuulize Maswali. Kuna pesa ya ushuru ambayo tunalipia wafanyikazi wetu. Pesa hii haijatufikia kwa kipindi cha miezi mitatu. Waziri hajawezesha pesa za kaunti ya Embu kufika ili wafanyikazi wa kaunti walipwe. Tungemwuliza swali hili iwepo angewasili Bungeni. Na sio kaunti ya Embu pekee, ila kaunti 47. Waziri Mbadi alisema hakuna pesa na angefika hapa ili tumuulize maswali. Naunga mkono kuwa Waziri Mbadi akuwe summoned aje Seneti kujibu maswali."
}