GET /api/v0.1/hansard/entries/1473430/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1473430,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1473430/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Wakati Waziri ameitwa na kukosa kuja tunaweza kumtetea, lakini si haki kwetu. Kama Sen. Munyi Mundigi alivyosema, pesa ya Embu imechelewa kwa muda wa miezi mitatu. Tungejua leo kama Waziri anajali maslahi ya watu wa Embu sio kutetea mwenye hakuja kujibu maswali. Hii ni kusema kuwa, Waziri anaridhika na hali ilivyo katika kaunti zetu zote 47. Kwa hivyo, sisi pia tusiende chini na kukubali kuwa tutakuwa tunakaa chini kama watu hawana kazi. Tukiita Waziri na haji, tuwe na sheria ambayo itaashiria uajibikaji. Kwa muda kumekuwa na madharau kwa Bunge la Seneti kutoka kwa Bunge la Kitaifa. Huu ukosefu wa adabu hautachukuliwa na Mawaziri. Tusiruhusu Mawaziri kutudharau wakati wanapoitwa kwenye Bunge hili."
}