GET /api/v0.1/hansard/entries/1473477/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1473477,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1473477/?format=api",
"text_counter": 142,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mutua",
"speaker_title": "The Cabinet Secretary for Labour and Social Protection",
"speaker": {
"id": 13137,
"legal_name": "Robert Mutemi Mutua",
"slug": "robert-mutemi-mutua"
},
"content": " Samahani, Bw. Naibu Spika. Shukran Sen. Madzayo kwa swali lako la kina kabisa. Kutokana na tukio hilo la ugaidi la mwaka wa 1998, wale walioumia walikuwa Wakenya na Wamarekani. Umesema kweli kuwa Marekani walioathiriwa walilipwa lakini Wakenya hawakulipwa. Hili ni swala ambalo nilifuatilia nikiwa Waziri wa Mambo ya Kigeni hata kwenye mikutano kadhaa tukiwa na Sen. Kavindu Muthama na wengine. Najua ya kwamba hivi sasa, kuna kesi inayoendelea kule Marekani. Pia, kuna juhudi za Wizara ya Kigeni kuona kama inaweza kudhibitshwa na kupitishwa na Bunge la Marekani ili waweze kulipwa. Kwa hivi sasa, sina uhakika hiyo kesi imefika wapi. Sen. Madzayo na Waheshimiwa, naomba mnipe nafasi niweze kumwandikia barua ndugu yangu, mhe. Musalia Mudavadi, ili aweze kutupa habari ili tuweze kufahamu mahali tumefika. Pia, nitalikaza na kuangalia vile tunaweza kujadiliana na wale walioumia ili tuweze kuwasaidia. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}