GET /api/v0.1/hansard/entries/1473480/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1473480,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1473480/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Serikali yetu ndio huwa inasajili watu na kutupatia hati ya kuzaliwa, kitambulisho, pasipoti na hata hati ya kifo wakati mtu ameaga dunia. Inakuwaje hamuwezi kuchukua takwimu ambazo ziko katika mitambo yenu siku ya leo ili kujua mtu ambaye amefikisha miaka ya kulipwa pesa zake za uzee? Je, ni lazima mrudi tena mkitumia fedha za umma kwenda kusajili watu na mko na kila kitu? Kwa sababu Serikali iko na kila kitu, ingekuwa rahisi mtu akitimiza ile miaka, mnachukua account yake na mnaanza kumtumia pesa zake moja kwa moja bila kusumbua wazee na vilema. Kwa nini kazi inafanyika hivyo? Ni nini hamna ya kufanya hiyo kazi ili iwe rahisi kwa kila mtu? Swali la pili---"
}