GET /api/v0.1/hansard/entries/1473867/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1473867,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1473867/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": null,
    "content": "wote. Wanakabiliana na masuala tofauti katika location zao, haswa elimu, mambo ya familia, na ardhi. Machifu hao lazima wawe na viwango vizuri vya masomo. Lazima waende shule. Mhe. Kamket ako na kitita kizima cha pesa za bursary cha kila mwaka wa kifedha. Wacha awarejeshe machifu wake shuleni wakasome ili waweze kuwahudumia watoto vizuri. Hatutawaweka machifu ambao hawajui kusoma na kuandika kuwasimamia watoto ambao wameenda shule, ama kuwahudumia wazazi wenye shida ambao wameenda shule. Masuala mengi yanayokumba jamii zetu yanahitaji mtu ambaye amesoma. Kwa hivyo, napinga suala hili la Mhe. Kamket kuwa machifu wakae bila masomo. Waende shuleni. Ahsante, Mheshimiwa Naibu Spika."
}