GET /api/v0.1/hansard/entries/1473871/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1473871,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1473871/?format=api",
"text_counter": 77,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii niunge mkono Statement ambayo imeletwa kwenye Bunge na Mhe. Kamket kuhusu mambo ya machifu . Tunaelewa kuwa machifu wanafanya kazi ambayo ni tofauti na nyingine katika nchi yetu ya Kenya. Huwezi kumuondoa chifu kutoka sehemu moja na kumpeleka kwa sehemu nyingine. Chifu si kama daktari, pilot ama mtendakazi yeyote wa Serikali. Kazi ya chifu ni kukaa katika sehemu anayoelewa sana. Kazi yake inahusu wananchi. Kwa hivyo, ukimpatia nafasi katika sehemu yake, atakuambia information kuhusu location na sub-location yake. Si lazima uwe umeenda shule ili upate information . Statement ya Mhe. Kamket haijasema machifu wasisome lakini isiwe lazima uwe na grade fulani ili upewe nafasi ya kuwa chifu. Hii ni kazi ambayo unafanya uliko. Hutoki hapo. Ikiwa Chifu angetaka kuendelea na masomo yake mpaka apate degree, hakuna mtu amemkataza. Hilo litakuwa jambo zuri, lakini lisihitajike wakati anaomba kazi. Cha muhimu ni chifu kuwa na elimu itakayomwezesha kufanya kazi yake pale nyumbani. Kazi hiyo ni ya maana sana kuliko yoyote ile, hata ya Wajumbe ambao wako hapa. Kazi ya chifu ni tofauti na zingine zile. Kwa hivyo, naunga mkono Mhe. Kamket, lakini hatujasema wasiende shule. Ni vyema waende shule. Mhe. mwenzangu kutoka Kilifi, naelewa kuwa eneo hilo ni remote area na kuna shida nyingi sana. Kuna shida kama zile zilizopo Kaunti za Turkana, Wajir na Mandera. Kule, watu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}