GET /api/v0.1/hansard/entries/1473891/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1473891,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1473891/?format=api",
"text_counter": 97,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
"speaker": null,
"content": " Mhe. Naibu Spika, naungana na Mbunge wa Malindi, Mhe. Amina Mnyazi kwa kauli hii. Huyu mwanaume wa takriban miaka arobaini amekuwa na hiyo tabia ndani ya Malindi na Watamu, Kaunti ya Kilifi. Huwa anatumia watoto wadogo. Amefanya hivyo mara nyingi. Amekimbia kwa muda sasa zaidi ya takriban miezi miwili. Wanasema hawajui yuko wapi. Hajatafutwa lakini asili yake ni Afrika Kusini, hapa karibu tu. Hajaenda mbali. Tunataka vyombo vya usalama, hasa ndani ya Kilifi Kaunti, kumtafuta mtu huyo. Watoto ambao amewatumia ni wadogo sana, chini ya miaka saba. Kuna hatari kwa sababu tunahofia magonjwa, hata yale ya kiakili kwa hao watoto. Trauma ni kitu ambacho hatuwezi kukubali ndani ya jamii, hasa kwetu. Wazazi wengi wametumika hasa katika hizo kesi nne ambazo tumezigundua na kufuatilia na Mhe. Amina. Wazazi wanatumika ambapo wanapewa Ksh2,000 na agent na wanaachilia watoto wao kupelekwa kwa huyo jamaa. Hakuna hatua ya kuridhisha ya kutafuta huyo Mwafrika kutoka kule Afrika Kusini. Tunahimiza na kupeana makataa atafutwe na afunguliwe mashtaka. Vile vile, hao watoto na wazazi wao ambao wameathirika kwa jambo hili walindwe. Watoto watafutiwe matibabu na haki zao zizingatiwe. Ahsante, Mhe Naibu Spika."
}