GET /api/v0.1/hansard/entries/1474213/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1474213,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1474213/?format=api",
"text_counter": 115,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante Bw. Naibu Spika. Kwanza, ni jambo la kusikitisha ikiwa utatoa taarifa ambayo haina ushahidi wowote kutumia jina la mtu mwengine ambaye hakupewa taarifa yoyote. Kama ingewezekana, pia yeye angeitwa kwa televisheni wakajibizana ili ijulikane nani ni mkweli au muongo. Lakini si vizuri kuchukua upande mmoja kutoa taarifa ya kushambulia upande mwengine. Watu wengine na wengi wetu tuliopo hapa kama ndugu yangu, Sen. Kinyua, ni mtu aliyetengeneza jina lake kule Laikipia kwa miaka mingi mpaka sasa amekuwa Seneta. Bw. Naibu Spika, pia wewe kule Meru, umetengeneza jina lako kamili, kwa hiyo itakuwa ni makosa mtu akitaja jina lako kwa ubaya bila wewe kupewa nafasi ya kujibu. Naungana na ndugu yangu, Sen. Cheruiyot, kwamba kuharibiana majina si haki. Onyo iende kwa wanahabari. Si vizuri kuchukua upande mmoja kulaumu upande mwengine. Tunakemea vikali kitendo hicho cha kuchafua majina ya watu. Si vizuri kuharibiana majina hususan kwa wanahabari wanaosambaza habari. Kwa mfano, Sen. Chute anajulikana sana katika Taifa la Kenya. Itakuwa si jambo zuri ajulikane kwa njia mbaya katika umri wake. Taarifa hiyo itakuwa imemharibia maisha yake yote."
}