GET /api/v0.1/hansard/entries/1474217/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1474217,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1474217/?format=api",
"text_counter": 119,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Ndio, niko barabarani kuelekea huko. Barabara ni ndefu sana. Tunalaani vikali kitendo kilichotendeka kwa taarifa ya habari. Nikirudi upande ule mwengine, ni jambo la kusikitisha vile vile kuona kwamba Kenya hii kuna watu wanaovaa magwanda ya kuficha sura na hatujui kama ni polisi ama majambazi. Kwa mfano, leo utapata mtu anakuja nyumbani kwako na humjui ni nani, na unapotoka kwa gari lako, anakuvamia na unatoweka. Tuliona kitendo hicho wakati Mhe. Alfred Keter alishikwa na polisi. Alishikwa akiwa barabarani wakati yeye ni mheshimiwa. Si jambo nzuri kwa Mkenya kushikwa kiholela akiwa Kenya. Nikija upande wa dada yangu, watu wake watatu wameshikwa na polisi. Familia yake imeenda kortini kudai wapendwa wao waachiliwe na polisi, lakini hadi wakati huu tunavyoongea, hao vijana watatu bado hawajaachiliwa na polisi. Bw. Naibu Spika, je kama ingekuwa ni mtoto wako, wangu, wa Sen. Chute au Sen. (Dr.) Khalwale? Saa hii familia hizi hazina raha ndani ya nyumba kwa sababu ya wapendwa wao kupotea."
}