GET /api/v0.1/hansard/entries/1474233/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1474233,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1474233/?format=api",
    "text_counter": 135,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, kulingana na ripoti iliyoletwa na Seneta Tobiko kuhusu watu kutekwa nyara, ningetaka kusema ya kwamba, Mkuu wa Polisi, Douglas Kanja, ameteuliwa rasmi. Anapaswa atokee kimasomaso ili aweze kupambana na haya mambo na aweze kuyakomesha. Hii ni kwa sababu, kuna sheria zinapaswa kufuatwa. Kama mtu ametenda kosa, ashikwe, apelekwe kortini na ahukumiwe. Hakuna kosa ambalo haliwezi kupewa adhabu yake. Tunapoongea hapa, mwakilishi wa Wadi ya Dela hajulikani alipo. Kwa sababu sasa tuko na askari mkuu aliyeteuliwa kirasmi, ana majukumu ambayo anapaswa awe akiangalia. Bw. Naibu wa Spika, si hiyo tu, Taarifa ililetwa na Seneta Okenyuri ya watu kuuwawa kiholela. Kazi kuu ya Serikali ni kulinda mali na maisha ya wananchi. Itakua ni jambo la kuvunja moyo sana ikiwa watu wanauliwa kiholela na familia zao zinaendelea kusononeka na hawapati jawabu ya yale mambo wanayoulizia. Vile vile, kuna Taarifa iliyoletwa na Seneta wa kutoka Uasin Gishu, kuhusu KCC. Wakulima wanaendelea kusononeka wakiuliza watapata malipo yao lini, ilhali wanaendelea kupeleka maziwa yao kule KCC. Ukitembea kule Nyahururu, kila wakati, asubuhi na mapema, watu wanapeleka maziwa yao KCC. Lakini, wakati wa kupata malipo yao, inakua ni mchongoma."
}