GET /api/v0.1/hansard/entries/1474588/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1474588,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1474588/?format=api",
    "text_counter": 107,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Tigania West, NOPEU",
    "speaker_title": "Hon. Mpuru Aburi",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii. Yangu ni kuunga mkono kamati ambayo ilitekeleza haya mambo kwa sababu Bw. Kanja ni mtu tunayemwelewa sisi Wakenya. Ukiangalia wakati alikuwa kwenye kitengo cha fanya fujo uone (GSU), alikuwa anazuia, haswa upande wa Meru, Tigania West, Igembe Central, Igembe North, wakati wa vita vya wizi wa ng’ombe. Yeye ni mtu ambaye ukimpigia simu wakati wowote hata kama hana nambari yako, ataichukua. Langu ni moja pekee, ni kusema kwamba katika kitengo cha polisi, watu wengi wanahaingaika. Ukiingia kwenye nyumba za polisi, wawili wanakaa kwenye nyumba moja yenye chumba kimoja, ilhali wana familia. Kanja akiingia pale kwa saa hizi, ataweza kuinua idara ya polisi."
}