GET /api/v0.1/hansard/entries/1475015/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1475015,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1475015/?format=api",
"text_counter": 55,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika. Swali langu kwa Bw. Waziri ni hili: Kumekuwa na malalamishi katika kaunti 47 kuhusu uajiri wa watu katika departments . Bw. Waziri, ulianza kazi juzi. Ningetaka kujua nini utafanya ili kila kaunti isherehekee keki ya Kenya nzima? Kumekuwa na shida ya internship kwa vijana wetu wale wamesoma. Kaunti nyingi zimekuwa na shida kwa sababu wale watu wako kwa department wakiajiri watu hawafanyi balancing . Sasa wewe kama Bw. Waziri mpya, utasaidiaaje? Jambo lingine, watu wengi wamepitisha miaka 60 na hawajaachishwa kazi. Tunajua vijana wetu wanataka kazi. Utasaidia namna gani ili vijana kila kaunti wapate kazi? Asante, Bw. Spika."
}