GET /api/v0.1/hansard/entries/1475135/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1475135,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1475135/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Naungana na Maseneta wenzagu kumpongeza Waziri wetu kwa uteuzi wake kwa mara ya pili. Hili ni thibitisho kuwa ni mkakamavu katika kazi yake. Swali langu ni hili; tunapojitayarisha kuadhimisha siku ya utalii ulimwenguni ambayo dhima yake ni utalii na amani, ni mikakati gani toka uingie katika ofisi hii mpya umeweka ili kuona kwamba anga ya Moi International Airport imefungulia ndege za kimataifa za kitalii kutua? Nilisimama mwaka jana na kumuuliza Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano swali hili lakini kukawa na mino mino na mivutano mingi. Ningependa kujua ni hatua gani umechukua kama Waziri kuona kwamba hizi ndege za kitaifa za kitalii zinaweza kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Moi pale Mombasa. Nasisitiza kuwa utalii ni uti wa mgongo wa gatuzi sita za pwani. Watalii wanapokosa kufika maeneo yetu inaashiria kwamba sisi kama wapwani tutaendelea kudidimia katika uchochole na watoto wetu watakosa nafasi za kazi ambazo tayari pale nyuma zilikuwa kabla ya janga la COVID-19. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}