GET /api/v0.1/hansard/entries/1475415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1475415,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1475415/?format=api",
    "text_counter": 196,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii nami nipate kuzungumza kuhusu NG-CDF. Katika maeneo bunge mengi, pesa za NG-CDF ndizo pesa pekee tunazotarajia kufanyia maendeleo. Eneo Bunge la Lamu Mashariki na maeneo bunge mengine mengi yamebaguliwa kwenye mipango ya maendeleo. Kwa mfano, tukiangalia rekodi, tutaona kwamba kwenye Bajeti ya mwaka uliopita, Eneo Bunge la Lamu Mashariki lilipewa Ksh4 milioni, ilhali kuna eneo bunge lingine ambalo lilipewa Ksh450 milioni. Pesa za NG-CDF ndizo pesa pekee ambazo hazihusishwi na ubabe kwa sababu kila eneo bunge linapata mgao wake na linajipangia miradi yake kulingana na jinsi sheria inavyosema. Katika Serikali kuu, pesa inakwenda mbio huku maeneo bunge mengine yakiendelea kubaki nyuma zaidi. Mbinu ya mambo yote ya Serikali inafaa iendelee kama ilivyo kupitia mpangilio wa NG-CDF. Niliupenda sana ule Mswada wa Fedha uliotupiliwa mbali kwa sababu ulikuwa unasema kila eneo bunge lipate Ksh50 millioni za kuwekeza kwenye miradi ya stima. Niliupenda Mswada huo kwa sababu angalau ulikuwa umetengea kila eneo bunge Ksh50 milioni. Pesa zilizobakia, kama walitaka kuzichezea msondo – ngoma inayochezwa kule kwetu – ni sawa tu! Wangezichezea. Angalau tulikuwa tumepata kitu cha kufuatilizia. Kupitia NG-CDF, angalau kila eneo bunge linaweza kupata pesa kiasi za kuanzishia miradi hata kama inabidi tufuatilie nyongeza kutoka kwa Serikali kuu. Ukiangalia kiasi cha fedha za Serikali kuu zinazoenda kwenye maeneo bunge yetu, utasikitika. Mfano mzuri ambao nimewapatia ni ule unaohusu nguvu za umeme . Angalieni rekodi muone jinsi pesa hizo zilivyokuwa zikigawanywa. Eneo Bunge la Lamu Mashariki halina hata inchi moja ya national grid. Mgao huo ukifuata mtindo wa NG-CDF, tuna uhakika kwamba kila mwaka tutapata Ksh50 milioni, na tungekuwa tumesonga mbele kidogo. Hivi sasa, tunasikitika, na inatuuma sana. Hatujui The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}