GET /api/v0.1/hansard/entries/1475566/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1475566,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1475566/?format=api",
"text_counter": 347,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": ", watasaidia taifa hili kwa mambo mengi sana, huku wakiingiza senti. Nikiangalia Kaunti ya Mombasa, naona vile vijana wameharibika. Ukiingia kwenye mitandao, unapata matusi tu na mambo mabaya. Kwa mfano, wanawatusi Waheshimiwa. Baadaye, mambo yanatokea ya kuharibu jamii na kukosanisha viongozi. Hiyo technopolis ikitolewa Konza na kuenea tupate hubs Mombasa, kwa Mhe. Irene Mayaka, ndugu yangu Kiarie na wengine, hao vijana wataitumia vizuri kutengeneza pesa na kufanya maendeleo. Hivi, watafungua uchumi wa Kenya ambao kwa wakati huu ni mbaya sana. Wakorea wakiangalia nchi yetu, wanaona technopolis iko Konza peke yake. Huu mwanya utafanya technopolis ziweze kuenea Kenya nzima na kusaidia vijana wote. Kwa ufupi, nauunga mkono Mswada huu ambao ni mzuri. Vijana wetu ambao wamekaa huku na huko, wataweza kufanya biashara, research na pia innovation ecosystems ili kutengeza vitu vizuri. Wao ni wasomi ila hawajapata mahali pa kutumia akili zao. Nataka kusema ahsante sana kwa ndugu yangu John Kiarie kwa kuwakumbuka vijana. Anajua vile akili zao zinaenda mbio. Wanahitaji mahali ambapo wataziweka, ili kuingiza senti na kuwacha kuwasumbua wazazi wao kule nyumbani. Hao vijana ndio wazazi wa kesho. Ukiwapatia hizo hubs, zitawasaidia sana."
}