GET /api/v0.1/hansard/entries/1475934/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1475934,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1475934/?format=api",
    "text_counter": 323,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Nilikuwa nachangia kauli hii nikisema ya kwamba, kuna miradi mingi ya maendeleo ambayo imekwama katika kaunti zetu. Kwa mfano, kuna kaunti ambazo miradi na mijengo imekwama kwa muda wa takriban miaka kumi, miaka sita na mingine miaka mitatu. Hatuoni sababu inayoshinikiza miradi hii kutokamilika. Ukipiga kurunzi, tunapata ya kwamba ni miradi ambayo huwapa mapato wanakandarasi ama baadhi ya maafisa katika kaunti husika. Hivi kuhakikisha ya kwamba Wakenya na wanakaunti wanakamuliwa pasipo wao kujua. Ninaunga Mhe. Sen. Kavindu Muthama mkono kwamba magavana na serikali za kaunti ziweze kujukumika. Wanapoanzisha miradi ya maendeleo, ikamilike katika awamu zao za uongozi ili wale ambao wanachukua hatamu za uongozi baadaye, wasilipe na kushugulika na madeni ambayo hawakuhusika kuidhinisha na kuanzisha."
}