GET /api/v0.1/hansard/entries/1475937/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1475937,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1475937/?format=api",
    "text_counter": 326,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, ni jambo ambalo linadhihirika kwamba miradi hii hupitishwa pasipo matarajio. Baadhi ya viongozi katika kaunti wanangoja hadi awamu ya mwisho wa mwaka wa bajeti, ama siku za kifedha, ndipo miradi hii kwa haraka hupitishwa katika awamu ya Supplementary Budgets . Mimi ninaomba Seneti iweze kumakinika na kuhakikisha ya kwamba mambo kama haya yanasitishwa na hatua madhubuti kuchukuliwa. Jambo la pili ni kuunga Mhe. Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, ya kwamba tutasitisha vikao nyetu ili kuhakikisha kwamba fedha ambazo kamati zinapewa ni za kutosha kuhakikisha ya kwamba kamati yetu inaenda nyanjani kushughulika na ukulima ambayo imegatuliwa kirasmi katika nchi ya Kenya. Hatuwezi kuwa tunakaa Nairobi kupiga gumzo na kuboronga Kingereza, kutunga sheria hapa Nairobi ilhali hatuendi mashinani ili wakulima wa mashinani wahusishwe katika sheria ambazo tunashughulikia. Juzi tulikuwa katika hatua za kufanya majadiliano ya Mswada kule Mombasa na tukakatisha safari yetu kwa sababu tuliambiwa kuwa mkoba wa kifedha wa Seneti umeisha na hakuna hela. Tukafunganya virago na kurudi Nairobi mioyo ikisononeka. Ilipaswa vile vile tuendelee na mikutano mingi. Mimi naomba kwa niaba ya wale ambao huenda wanaumia na wameshindwa kuzungumza, kusema kwamba kamati za Bunge zipewe fedha za kutosha. Tukiangalia Seneti katika miaka iliyopita, walikuwa wanapewa fedha za kutosha kufanya kazi. Mimi ninaomba turudi katika kumbukumbu za kifedha na tuone. Iwapo miaka kumi iliyopita The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}