GET /api/v0.1/hansard/entries/1475938/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1475938,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1475938/?format=api",
"text_counter": 327,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "kamati ilikuwa inapewa pesa, kwa mfano, shilingi milioni 20 au 15, itakuwaje sasa wakati ambapo tumepiga hatua nyingi za kigatuzi tunaanza kukohoa na kukatiwa hewa ya kifedha. Hili ni jambo ambalo viongozi katika Bunge hili na viongozi katika kamati za Seneti, wamakinike, wajinyanyue na watutetee kwa sababu tumewapa nafasi. Hatutarajii sisi wenyewe tuje hapa, tuanze kuzusha na kudai kana kwamba sisi sio Seneti ambalo hugawia kaunti fedha za ugatuzi za kufanya maendeleo. Juzi tulipitisha shilingi 400 bilioni kuenda katika kaunti zetu. Iwaje sisi wenyewe tunashindwa kutekeleza majukumu yetu kwa sababu hatuna pesa? Ni kinaya. Ninataka nielezwe kama kuna pesa ama hakuna pesa. Huenda ninasema hakuna pesa ilhali ziko hewani mahali na sijaziona. Bw. Naibu Spika, ninashukuru kwa nafasi hii na kutaraji kwamba miradi ambayo haijakamilika ikamilike na ile ambayo yanapaswa kuanza yaanzishwe na imalizwe katika awamu za magavana waliyoko sasa."
}