GET /api/v0.1/hansard/entries/1475957/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1475957,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1475957/?format=api",
    "text_counter": 346,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ninasimama kuunga mkono taarifa iliyowasilishwa na Seneta wa Machakos, Sen. Kavindu Muthama, kuhusu miradi ambayo imekwama katika kaunti zetu. Kwa hakika, miradi mingi imekwama na kutotimiza kazi ambayo ilianzishwa kufanya kwa sababu ya viongozi waliokuwa hapo awali. Kwa mfano, kama ni gavana, akipata mradi ambao ulianzishwa na gavana aliyemtangulia ama kama ni Mbunge au mwakilishi wadi, wanaacha hiyo miradi kwa sababu za kisiasa. Wanaona wakimaliza, atakaye pata sifa ni yule aliyetangulia kuaazisha huo mradi, ambayo ni makosa. Jambo la pili ni kusema kwamba pesa za umma zinatumika kuanzisha hii miradi. Miradi hiyo isipokamilika ndio iwafaidi wananchi, basi pesa za umma zinapotea na kuwa"
}