GET /api/v0.1/hansard/entries/1475959/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1475959,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1475959/?format=api",
    "text_counter": 348,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Beth Syengo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": ". Ni makosa sana kwa pesa za umma kupotea na kukosa kufaidi wananchi. Bw. Naibu Spika, miradi ikianzishwa katika kaunti zetu na kukosa kukamilika au kutumika, basi inakuwa maendeleo yamesimama. Tujuavyo kama viongozi katika Seneti, sisi hutetea ukamilifu na ufanyakazi kwa ugatuzi. Kwa hivyo isipofanyika, basi inakuwa kwamba kazi yetu haijahalalishwa kikamilifu. Wananchi wa Kenya wanapoteza pesa zao, maendeleo yanakosa kupatikana mashinani. Wananchi wanahangaika ilhali walipiga kura na wanalipa ushuru. Pesa ambazo wanatoa kwa kulipa ushuru zinapaswa kutimika kuleta maendeleo kwa wananchi. Kukosa maendeleo ni kupoteza pesa za wananchi jambo ambalo halistahili. Bw. Naibu Spika, nitachangia kidogo kuhusu ripoti iliyoletwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. Mimi ni mwanakamati wa Kamati ya Kilimo na Mifugo. Ni vibaya kwamba mgao wa fedha unaopaswa kuenda kwa Kamati ya Kilimo na Mifugo---"
}