GET /api/v0.1/hansard/entries/1476030/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476030,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476030/?format=api",
    "text_counter": 419,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, nasimama kuunga mkono ripoti iliyoletwa na Kamati ya Fedha na Bajeti inayoashiria kwamba tusipunguze pesa zinazoenda kwenye gatuzi zetu kutoka shilingi 400 bilioni mpaka shilingi 380 bilioni. Lazima tutofautishe kati ya pesa ambazo tunapeleka kwa gatuzi zetu za Kenya na yale ambayo yanakuja. Ndio maana tuko na kamati mbili; moja ikiwa ya County Public Accounts Committee (CPAC) na ingine ya PICSF za kuangalia kwamba kila kaunti inatumia pesa zake inavyostahili. Siku ya leo, tumekuwa na ripoti nyingi. Nimekuwa na ripoti ambayo imetoka kwa Kamati ya CPAC na nikasoma kuhusu vile Kaunti ya Kirinyaga inatumia pesa na mahali wanafaa kurekebisha. Kuna mambo mengi ambayo hayajafanyika katika gatuzi zetu. Utapata barabara bado hazijatengenezwa na hospitali zetu hazina madawa. Kuna baadhi ya watoto wetu ambao hawajapata bursary wanavyopaswa kupata. Pia, malipo ya walimu wengi, sana sana wa shule za chekechea, ni duni katika gatuzi zingine. Kwa hivyo, Bunge la Taifa kusema kwamba tupunguze pesa za kaunti kutoka shilingi bilioni 400 hadi shilingi bilioni 380 ni makosa na dhuluma kwa kaunti zetu. Tunatarajia mambo yatakuwa mazuri, hasa upande wa kilimo na ndio maana tulipitisha Mswada wa kuongeza pesa hizo hadi shilingi bilioni 400. Nilikuwa natarajia kwamba kutakuwa na mabadiliko ili kusaidia wakulima kwa sababu ya pembejeo. Pisa hizo zilifaa kuwasaidia wakulima wa ng’ombe wa maziwa na majani chai ili waweze kuendeleza kilimo chao. Kwa hivyo, tukipunguza, tutapatia kaunti zetu sababu za kusema kwa nini hawakuweza kufanya hivyo. The Division of Revenue Act (DORA) inasema kwamba kunapokuwa na upungufu wakati wa kukadiria bajeti, Serikali kuu itawajibika kujaza pengo ambalo litakuwa limeachwa wakati wa bajeti ya ziada. Kwa hivyo, siyo haki kupunguza pesa za kaunti kwa kiwango hicho ambacho kinapendekezwa na Bunge la Taifa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate."
}