GET /api/v0.1/hansard/entries/1476031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1476031,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1476031/?format=api",
    "text_counter": 420,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Kazi kubwa ya Seneti ni kulinda ugatuzi na ndio maana tuko hapa. Kulinda ugatuzi ni kuhakikisha kwamba fedha zinazokusudiwa kwenda katika kaunti zetu zinatumwa ipasavyo. Tushavalia njuga suala hili kwa sababu tuliketi na kupitisha. Kwa hivyo, naomba pesa ziende mashinani jinsi tulivyokuwa tumesema. Bw. Spika wa Muda, napinga kupunguzwa kwa fedha ambazo zitaenda katika kaunti zetu. Naunga mkono ripoti ilioletwa hapa na Kamati ya Seneti ya Fedha na Bajeti kusema kwamba fedha zitakazoenda katika kaunti zetu zibaki shilingi bilioni 400 wala siyo shilingi bilioni 380. Pesa hizo zinapoenda kule, tunaomba magavana wawajibike. Kama kuna watu waastarabu ni Maseneta. Tunatetea na kupitisha pesa za kwenda katika kaunti zetu ilhali hatuhusishwi katika kujua jinsi zinavyotumika. Heshima tunayoweza kupewa na kaunti zetu ni kuhakikisha kwamba wanatumia pesa tunazopigania kwa njia inayofaa kufikia “Wanjiku”. Kikwetu, kuna msemo kuhusu anayekama na yule anayetoa kombamwiko kwenye maziwa ili watoto wanywe. Sisi Maseneta tushafanya kazi ya kukama. Magavana na Wawakilishi wa Wadi wanatoa tu kombamwiko kwenye maziwa ili wakazi wajivunie matunda ya ugatuzi na kupata huduma inavyopaswa. Kwa hayo mengi, Bw. Spika wa Muda, naunga mkono ripoti ya Kamati ya Fedha na Bajeti."
}